Kusambaza umeme Kivu Kaskazini

Ku boresha maisha ya kila siku

Kwa mwisho wa mwaka 2023, Zaidi ya manyumba 30,000 zime pewa umeme wa Virunga Energies huku zaidi ya watu 140,000 ku faidika na mpango huu. Ni mara ya kwanza kiasi hiki cha manyumba kupata umeme jimboni na maisha ya kila siku ku boreshwa.

Umeme kwa viwanda vya maji

Kupata maji bora ya kunywa

Kwa mwaka wa 2020, Virunga Energies ali towa umeme kwa kiwanda moja cha maji eneo za magharibi ya mji wa Goma naku raisisha kupata maji kwa wakaaji 300 000. Viwanda vya maji vingine vitatu vita pewa moto na kwa mwisho wa mpango huu, watu zaidi ya milioni moja wata rahisishwa kupata maji safi.

Mwezi wa tisa mwaka wa 2023, mradi wa usambazaji wa maji katika eneo la Nyiragongo ulizinduliwa. Zaidi ya jamii 150,000 zimefaidika na mradi huu ulio saidiwa kipesa na Umoja wa Ulaya, ambao mpango wake wa pili ilianzishwa mwezi wa Januari 2024. Kwa jumla visima 14 vipya vya maji vimeanzishwa pa mtaa wa nyiragongo  kwa ajili ya jamii za wakimbizi na wenyeji wa eneo hilo.

Umeme wa bure

Kuboresha huduma za kijamii

Virunga Energies ya boresha huduma za kijamii kupitia ku pana umeme kwa bure kwenye ma hospitali, ofisi za serikali, shule, na vituo vya radio zaki jamii. Kwa sasa vituo zaidi ya 20 vya faidika na mpango huu pa Goma, Rutshuru, Nyiragongo, Mutwanga na Lubero.

Wakaaji wote wa miji na vijiji vinavyo kua na umeme wa Virunga Energies wa faidika na taa za barabarani. Kutokana na mpango huu, usalama waboreshwa kwa wanao tembea usiku na kuendesha biashara ndogo ndogo. Ku boreshwa kwa usalama ndani ya maeneo yanao faidika na taa za barabarani wa shuhudiwa hasa hasa na wanawake wano kutana na changamoto za ubakaji na kubebwa porini.

Kukuza uchumi

Kusaidia biashara

Maendeleo ya kampuni ndogo naza kati haiwezekani bila umeme bora. Umeme wa jenereta, mbali yakuwa siyo bora kwa mazingira, ina beyi kali sana. Mwishoni mwa mwaka 2023, kampuni 1611 zatumia umeme wa Virunga Energies na kuwa chemchemi ya kazi kwa wakaaji.

Zaidi ya umeme bora na yaku aminika kwa baazi ya makampuni, Virunga Energies ya sindikiza ma kampuni zinazo tumia umeme wake ndani ya hatua zaku kupata mikopo. Wanao faidika na mpango huu wa lipa mkopo kupitia kununua umeme. Mwishoni mwa mwaka 2021, kampuni 367 za mahali zime faidika na mpango huu.

Viwanja 2 vya viwandani pia vime tengenezwa. Ndani ya viwanja hivi, kampuni hupata mazingira bora kwa maendeleo yao, salama ya vifaa, u raisi wa kupata umeme na maji, pamoja na miundombinu ya kituo cha kuwasaidia kuanzisha shughuli zao. Kampuni zilizopo ndani ya viwanja hivyo za pata pia mafunzo na ushauri wa kifedha.