Virunga Energies ya pana umeme yenye kuheshimu mazingira, yenye ku aminika na kwa bei rahisi kwa wakaaji wanaoishi ndani na kando ya mbuga la wanyama la Virunga.

Virunga Energies ina mpango waku gawa umeme ndani ya miji mikuu kenda ya jimbo la kivu Kaskazini ili ku boresha maisha na uchumi kwa manufaa ya watu zaidi ya milioni 3.8. Kwa hiyo, Virunga Energies inaaendesha mwenyewe kazi za ujenzi wa viwanda na singa za umeme, ugawaji na uuzaji wa moto mpaka kwa mtumiaji wa mwisho.

Kwaku fikia lengo lake, Virunga Energies ina mpango waku zalisha kiasi cha Megawati 100 kabla mwaka 2040. Kwa sasa, kupitia viwanda vyake vya moto (Mutwanga, Matebe na Luviro), Virunga Energies ya zalisha tayari megawatt 30. Ujenzi wa kiwanda mpya (Rwanguba) waendeshwa huku kukitarajiwa kuzalishwa megawatt 30 zaidi.

  • 30,663 nyumba zime pewa umeme

  • 1,611 byashara zime pewa umeme

  • Ugawaji wa maji safi ku boreshwa kwa wakaaji 300,000

  • Taa za barabarani kuwekwa ndani ya mji na vijiji 20 na katika mji mkuu wa Goma

Kazi Zetu

  • Ujenzi wa viwanda vya umeme

    Kwa sasa, Virunga Energies imejenga na kuendesha viwanda vya moto vi tatu mu kiwemo : Mutwanga, megawati 1.4, Matebe megawati 13.1 na Luviro, megawati 14.6.

    Ujenzi wa kiwanda kingine waendeshwa pa Rwanguba kando ya Matebe, kiwanda hiki cha tarajiwa kuzalisha nguvu kiasi ya megawati 30 (megawati 15 zita zalishwa kwa awumu ya kwanza). Kazi za ujenzi zime anzishwa na zita enda ziki ongezeka hatua kwa hatua.

  • Ugawaji wa umeme

    Kwa kugawa umeme kutoka viwanda vyake vya moto, Virunga Energies ime jenga njia za volti za kati na za chini ndani ya mtaa wa Rutshuru, Nyiragongo, Beni na Lubero pia ndani ya mji wa Goma. Kampuni Virunga Energies yaendelea ku kuza mtandao wake wa umeme ili kusambaza maeneo mapya na hivyo kujibu kwa mahitaji makubwa ya umeme.

  • Uuzishaji wa moto

    Virunga Energies hu uza umeme moja kwa moja kwa watumiaji kupitia mita za kulipia kabla. Wafanyakazi wa virunga wana jukumu la kutafuta wateja wapya na kuwasaidia katika mchakato waku pata umeme.

    Mnamo 2023, Virunga Energies ilisambaza umeme kwa zaidi ya wateja 32,000.

Timu Yetu

Virunga Energies has qualified, young and dynamic staff to carry out its mission. Agents are assigned across various sites of the company in Goma, Beni, and Lubero.

Fungua