Virunga Energies SAU iliundwa mwaka wa 2013. Kampuni inamilikiwa na Virunga Foundation inayoongoza mbuga la wanyama la Virunga kwa sasa. Kazi kuu za Virunga Energies niku jenga viwanda vya umeme, kugawa moto, na kuuza wa umeme safi kwa ajili ya kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa watu wanao ishi kando ya mbuga la wanyama la Virunga.
Virunga Energies ni kampuni yaki biashara inayo kuwa na malengo ya kijamii. Mapato yake hutumika kulipa gharama zake za uendeshaji na matengenezo ya vifaa vyake, kutekeleza misheni yake ya utumishi wa umma (haswa taa za barabarani) na kuongeza uwezo wake wa uzalishaji pia na mtandao wake wa umeme. Kiasi kilichowekezwa tangu 2013 kinazidi $120m. Kama mwanzilishi wa modeli mpya ya ugawaji wa umeme, kampuni Virunga Energies ili nufaika na mkopo wa kwanza kutoka benki ya uwekezaji mashariki mwa DRC.
Kwa sasa, kampuni ipo katika maeneo ya Beni, Lubero, Rutshuru, Nyiragongo na katika mji mkuu wa Goma.
Tangu kuanzishwa, Virunga Energies imenufaika na usaidizi wa kifedha kutoka Umoja wa Ulaya, The Schmidt Family Foundation, The World We Want na British international Investistment.