Maendeleo ya kampuni ndogo naza kati haiwezekani bila umeme bora. Umeme wa jenereta, mbali yakuwa siyo bora kwa mazingira, ina beyi kali sana. Mwishoni mwa mwaka 2023, kampuni 1611 zatumia umeme wa Virunga Energies na kuwa chemchemi ya kazi kwa wakaaji.
Zaidi ya umeme bora na yaku aminika kwa baazi ya makampuni, Virunga Energies ya sindikiza ma kampuni zinazo tumia umeme wake ndani ya hatua zaku kupata mikopo. Wanao faidika na mpango huu wa lipa mkopo kupitia kununua umeme. Mwishoni mwa mwaka 2021, kampuni 367 za mahali zime faidika na mpango huu.
Viwanja 2 vya viwandani pia vime tengenezwa. Ndani ya viwanja hivi, kampuni hupata mazingira bora kwa maendeleo yao, salama ya vifaa, u raisi wa kupata umeme na maji, pamoja na miundombinu ya kituo cha kuwasaidia kuanzisha shughuli zao. Kampuni zilizopo ndani ya viwanja hivyo za pata pia mafunzo na ushauri wa kifedha.