Utaratibu wa kuunganisha ni mfupi na bei ni rahisi ili kuwezesha idadi kubwa ya kampuni kupate umeme. Ili kufaidika na muunganisho, masharti yafuatayo lazima yakamilishwe:
- Kampuni (Kiwanda) kuwa kwa umbali usio zidi 50m na nguzo ya kugawa umeme (Poteau de raccordement)
- Kusaini kibarua cha kuomba umeme
- Kuonesha kikaratasi toka ofisi jimboni ya Umeme kinacho ruhusu uchukue umeme
- Kuonyesha karatasi ya utambulisho na umiliki wa udongo (pièce d’identité, titre d’occupation parcellaire) pia na mchoro wa namna ufungaji wa umeme ume fanyika (schéma unifilaire)
- Kuwa na uwezo waku lipa pesa ili kupata umeme
* Kwa zaidi ya mita 50 za umbali, uunganisho inawezekana kwa kulipa gharama ya zaidi