Virunga Energies ya pana umeme yenye kuheshimu mazingira, yenye ku aminika na kwa bei rahisi kwa wakaaji wanaoishi ndani na kando ya mbuga la wanyama la Virunga.

Virunga Energies ina mpango waku gawa umeme ndani ya miji mikuu kenda ya jimbo la kivu Kaskazini ili ku boresha maisha na uchumi kwa manufaa ya watu zaidi ya milioni 3.8. Kwa hiyo, Virunga Energies inaaendesha mwenyewe kazi za ujenzi wa viwanda na singa za umeme, ugawaji na uuzaji wa moto mpaka kwa mtumiaji wa mwisho.

Kwaku fikia lengo lake, Virunga Energies inakusudia kuzalisha hadi MW 100 ifikapo 2040. Virunga Energies tayari ina uwezo wa uzalishaji wa ~ 43 MW na inatarajia kuagiza turbine ya pili huko Rwanguba kwa uzalishaji wa ziada wa MW 14.

  • 42,400 nyumba zime pewa umeme

  • 2,800 byashara zime pewa umeme

  • Ugawaji wa maji safi ku boreshwa kwa wakaaji 700,000

  • Taa za barabarani kuwekwa ndani ya mji na vijiji 20 na katika mji mkuu wa Goma

Kazi Zetu

  • Ujenzi wa viwanda vya umeme

    Virunga Energies imejenga na kuendesha, hadi sasa, mitambo 4 ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji ikiwa ni pamoja na: Mutwanga katika Beni, MW 1.4, Matebe katika Rutshuru MW 13.1 na Luviro katika Lubero 14.6 MW na Rwanguba katika Rutshuru 14 MW (inasubiri kukamilika kwa awamu ya pili ambayo 124 inatarajiwa kuzalisha MW 2 za ziada).

  • Ugawaji wa umeme

    Kwa kugawa umeme kutoka viwanda vyake vya moto, Virunga Energies ime jenga njia za volti za kati na za chini ndani ya mtaa wa Rutshuru, Nyiragongo, Beni na Lubero pia ndani ya mji wa Goma. Kampuni Virunga Energies yaendelea ku kuza mtandao wake wa umeme ili kusambaza maeneo mapya na hivyo kujibu kwa mahitaji makubwa ya umeme.

  • Uuzishaji wa moto

    Virunga Energies hu uza umeme moja kwa moja kwa watumiaji kupitia mita za kulipia kabla. Wafanyakazi wa virunga wana jukumu la kutafuta wateja wapya na kuwasaidia katika mchakato waku pata umeme.

    Mnamo 2025, Virunga Energies ilisambaza umeme kwa zaidi ya wateja 42,000.

Timu Yetu

Virunga Energies ina wafanyakazi waliohitimu, vijana na mahiri kutekeleza dhamira yake. Mawakala hutumwa katika tovuti mbalimbali za kampuni huko Goma, Rutshuru, Beni na Lubero.

Fungua